Psalms 16

Sala Ya Matumaini

Utenzi wa Daudi.

1 aEe Mungu, uniweke salama,
kwa maana kwako nimekimbilia.

2 bNilimwambia Bwana, “Wewe ndiwe Bwana wangu;
pasipo wewe sina jambo jema.”
3 cKwa habari ya watakatifu walioko duniani,
ndio walio wa fahari ambao ninapendezwa nao.
4 dHuzuni itaongezeka kwa wale
wanaokimbilia miungu mingine.
Sitazimimina sadaka zao za damu
au kutaja majina yao midomoni mwangu.

5 e Bwana umeniwekea fungu langu na kikombe changu;
umeyafanya mambo yangu yote yawe salama.
6 fAlama za mipaka zimeniangukia mahali pazuri,
hakika nimepata urithi mzuri.

7 gNitamsifu Bwana ambaye hunishauri,
hata wakati wa usiku moyo wangu hunifundisha.
8 h iNimemweka Bwana mbele yangu daima.
Kwa sababu yuko mkono wangu wa kuume,
sitatikisika.

9 jKwa hiyo moyo wangu unafurahia, na ulimi wangu unashangilia;
mwili wangu nao utapumzika salama,
10 kkwa maana hutaniacha kaburini,
wala hutamwacha Mtakatifu Wako kuona uharibifu.
11 lUmenijulisha njia ya uzima;
utanijaza na furaha mbele zako,
pamoja na furaha za milele
katika mkono wako wa kuume.
Copyright information for SwhNEN